Ghasia zaugubika uchaguzi Nigeria | Matukio ya Kisiasa | DW | 10.04.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Ghasia zaugubika uchaguzi Nigeria

Bomu limelipuka katika kituo kimoja cha kuhesabia kura huko nchini Nigeria ambapo msemaji wa shirika la dharura la nchi hiyo amesema watu kadhaa wamejeruhiwa vibaya.

default

Watu wakipiga kura Nigeria

Bomu hilo liliripuka wakati maafisa wa tume ya uchaguzi walipokuwa wakihesabu kura kufuatia uchaguzi wa bunge hapo jana Jumamosi. Shambulio hilo linafuatia mengine kadhaa hapo Jumamosi na Ijumaa.

Makundi yanayohusika na masuala ya haki za binaadamu yanakadiria kuwa zaidi ya watu 80 wamekwishauawa kutokana na ghasia za kisiasa nchini Nigeria tokea mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka jana.

Baada ya kuahirishwa mara mbili kutokana na matatizo ya kiutawala, hatimaye uchaguzi huo ulifanyika hapo jana na utafuatiwa na ule wa urais wiki ijayo kabla ya kufanyika wa magavana wa majimbo yote 36 ya Nigeria tarehe 26 mwezi huu.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/ZPR

Mhariri:Grace Kabogo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com