Ghasia za uchaguzi nchini Kenya | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 26.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

IDHAA YA KISWAHILI

Ghasia za uchaguzi nchini Kenya

---

NAIROBI

Maafisa wawili wa polisi wameuwawa na wengine wengi wamejeruhiwa na kundi la watu wanaodai polisi hao walikuwa wakipanga njama za kuiba kura katika uchaguzi wa hapo kesho.Kundi hilo la watu limedai polisi wanataka kufanya mizengwe kumpendelea rais Mwai Kibaki katika uchaguzi.Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na msemaji wa Polisi nchini humo bwana Eric Kirathe wawili hao waliouwawa walikuwa ni miongoni mwa mamia ya polisi waliopelekwa kuweka amani katika uchaguzi mkoani nyanza katika wilaya ya Suba kilomita 300 kutoka mji mkuu Nairobi.Tukio hilo limeripotiwa kufanyika jana usiku.Aidha hapo jana mgombea wa urais kutoka upande wa upinzani bwana Raila Odinga alidai kwamba polisi wanatumiwa kuiba kura hapo kesho.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com