GAZA:Hamas na Ffatah kubadilishana wafungwa wa kivita | Habari za Ulimwengu | DW | 31.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA:Hamas na Ffatah kubadilishana wafungwa wa kivita

Vikundi hasimu huko Palestina vya Hamas na Fatah vimekubaliana kubadilishana wafungwa waliyokamatwa katika mapambano kati ya vikundi hivyo huko ukanda wa Gaza.

Hatua ni kati ya makubaliano ya kusitisha vita yaliyofikiwa jana usiku, makubaliano ambayo yanaonekana kutekelezwa pamoja na kuawa kwa kamanda wa kikundi cha Hamas.

Hamas inaituhumu Fatah kwa mauaji hayo yaliyotokea katika mji wa Khan Younis.

Mapigano ya hivi karibuni kati ya vikundi hivyo yamepeleka vifo vya zaidi ya watu 30 na kufifilisha juhudi za Rais wa Mamlaka ya wapalestina Mahmoud Abbas za kuundwa kwa serikali ya kitaifa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com