Gaza. Wapalestina watatu wauwawa na jeshi la Israel. | Habari za Ulimwengu | DW | 27.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Gaza. Wapalestina watatu wauwawa na jeshi la Israel.

Jeshi la Israel limewauwa Wapalestina watatu katika matukio tofauti katika ukanda wa Gaza.

Wapalestina wawili wameuwawa katika mapigano ya risasi katika matukio mawili karibu na mji wa Khan Younis na wa tatu ameuwawa karibu na Beit Hanoun.

Jeshi la Israel limesema kuwa watu hao wamekuwa wakionyesha vitendo vya kutia mashaka wakati walipopigwa risasi na kuuwawa.

Israel imekuwa ikifanya mashambulizi katika ukanda wa Gaza tangu pale alipokamatwa mmoja wa wanajeshi wake hapo Juni 25 na kundi la wapiganaji.

Mwanajeshi huyo bado anashikiliwa na kundi hilo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com