Eu watilia shaka uchaguzi wa Kenya | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 01.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Eu watilia shaka uchaguzi wa Kenya

---

NAIROBI

Kiongozi wa ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya katika uchaguzi wa Kenya,bwana Alexander Lambsdorf leo amekosoa vikali jinsi uchaguzi wa Kenya ulivyokwenda akigusia zaidi namna matokeo ya urais yalivyokuwa yakitolewa.Katika ripoti ya mwanzo juu ya uchaguzi huo waangalizi wa uchaguzi huo kutoka Umoja wa Ulaya wamesema kulikuwa na dosari na uchaguzi war ais haukufikia viwango vya kimataifa.Aidha Kiongozi wa ujumbe huo Alexender Lambsdorf ameelezea kusikitishwa kwake na jinsi waangalizi wa kimataifa walivyokuwa wakizuiliwa kufanya kazi zao katika vituo mbali mbali vya kupigia kura na hata kuzuiliwa kuingia katika ukumbi wa kuhesabu kura.Wakati huohuo maduka na biashara bado zimefungwa nchini Kenya huku kukiwa na upungufu wa vyakula ingawa machafuko yameripotiwa kupungua.Taarifa zinasema ghasia za siku tatu nchini humo zimesababisha vifo vya watu kiasi cha 200.Kiongozi wa Upinzani wa chama cha ODM bwana Raila Odinga hapo jana aliwalaumu maafisa wa polisi wa serikali kwa ghasia na mauaji ya watu yaliyotokea na kutangaza mipango ya kufanyika maandamano makubwa ya amani.

Maandamano yamepangwa kufanyika alhamisi ili kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi rais Mwai Kibaki ambaye aliapishwa muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi. Hapo jana pia makamishana 4 wa ngazi ya juu wa tume ya uchaguzi wametaka paundwe tume huru itakayochunguza madai ya kufanyika mizengwe katika matokeo ya uchaguzi huo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com