Ethiopia yakikaribisha kikosi cha Umoja wa Afrika kwa muda | Habari za Ulimwengu | DW | 11.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ethiopia yakikaribisha kikosi cha Umoja wa Afrika kwa muda

Ethiopia imekubali kukikaribisha kikosi cha Umoja wa Mataifa kwa muda kilinde mpaka kati yake na Eritrea baada ya serikali ya mjini Asmara kukatiza usafirishaji wa mafuta kwa kikosi hicho.

Wizara ya mashauri ya kigeni ya Ethiopia imesema kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa hata hivyo hakitaruhusiwa kufanya harakati za aina yoyote ila kitakuwa na jukumu la uongozi.

Baraza la usalama la Umoja wa Mafaifa lilirefusha mamlaka ya tume ya umoja huo katika mpaka wa Ethiopia na Eritrea kwa miezi sita, lakini haikuwa wazi kikosi hicho kingeweza kukaa kwa muda gani kutokana na hatua ya Eritrea kukatiza usafirishaji wa mafuta.

Eritrea imesema kuwepo kwa majeshi ya kulinda amani katika eneo la mpakani ni sawa na kukalia nchi hiyo na imepuuza tarehe ya mwisho iliyowekwa na Umoja wa Mataifa iwapelekee mafuta wanajeshi hao.

Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi, amemhakikishia katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, kwamba atashirikiana na kikosi cha umoja huo kukabiliana na chanagamoto ya sasa dhidi yake, ikiwa ni pamoja na kukiruhusu kikosi hicho kikae kwa muda nchini Ethiopia.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com