DILI: Jose Ramos-Horta ashinda uchaguzi wa urais Timor Mashariki.
10 Mei 2007Matangazo
Mshindi wa Tuzo ya amani ya Nobel, Jose Ramos-Horta ameshinda uchaguzi wa kwanza wa urais katika Timor Mashariki.
Tume ya uchaguzi imetoa matokeo ya awali yaliyoonyesha Jose Ramos-Horta ameshinda asilimia sabini na tatu ya kura kati ya asilimia tisini ya kura zilizohesabiwa.
Jose Ramos-Horta ameahidi atajitahidi kuleta umoja katika Timor Mashariki.
Uchaguzi huo ulilengwa kumchagua mtu atakayechukua mahali pa Rais Xanana Gusmao.
Uchaguzi huo ndio wa kwanza nchini Timor Mashariki tangu mwaka 2002 miaka mitatu baada ya nchi hiyo kupata uhuru wake kutoka Indonesia.