1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Copenhagen. Jengo la vijana lavunjwa.

5 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCM6

Nchini Denmark , polisi wanalinda kundi la wabomoaji ambao wameanza kazi ya kuvunja jengo lenye ghorofa nne la kituo cha vijana mjini Copenhagen ambacho kimekuwa katikati ya machafuko ya mitaani ya hivi karibuni.

Zaidi ya watu 600 wamekamatwa katika siku mbili za machafuko ambazo yamezuka kuanzia siku ya Alhamis usiku baada ya polisi wenye silaha kuingia katika jengo hilo na kutaka kuwaondoa watu wanaoishi katika jengo hilo. Kundi la kidini la Kikristo ambalo lilinunua nyumba hiyo mwaka 2000 limeshindwa mara mbili kuwaondoa watu hao kwa hukumu ya mahakama. Watu hao wanaliona jengo hilo kuwa nyumba ya bure ya kuishi. Jengo hilo pia ni sehemu ya watu kukutana wakiwa na malengo mbali mbali ya kisiasa.