Conakry:Viongozi wa wafanya kazi nchini Guinea wanakataa kufanya mazungumzo na serekali hadi amri ya kijeshi imeondoshwa nchini | Habari za Ulimwengu | DW | 18.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Conakry:Viongozi wa wafanya kazi nchini Guinea wanakataa kufanya mazungumzo na serekali hadi amri ya kijeshi imeondoshwa nchini

Katika nchi ya Afrika Magharibi ya Guinea, viongozi wa vyama vya wafanya kazi wamekataa kufanya mazungumzo yenye nia ya kuikomesha michafuko hadi pale rais wa nchi hiyo, Lansana Conte, atakapoifuta sheria ya kijeshi katika nchi hiyo. Zaidi ya watu 100 wameuwawa katika michafuko ilioanza baada ya kuitishwa mgomo mkuu hapo Januari 10. Mashahidi na jumuiya za kupigania haki za binadamu zimelilaumu jeshi la nchi hiyo kwa kuwashambulia raia na kupora mali baada ya sheria ya hali ya hatari kutangazwa jumatatu iliopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com