CAIRO:Vijana waathirika sana na matumizi ya dawa za kulevya | Habari za Ulimwengu | DW | 03.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CAIRO:Vijana waathirika sana na matumizi ya dawa za kulevya

Utafiti rasmi nchini Misri unaonyesha kuwa yapata asilimia 8.5 ya idadi ya watu wan chi hiyo wana tatizo la kutumia dawa za kulevya.Kiwango hicho ni sawa na watu milioni 6.Utafiti wa hivi majuzi uliochapishwa na Baraza la kupambana na matumizi ya dawa za kulevya NCFTA wengi ya wanaoathiriwa ni vijana walio na umri kati ya miaka 15 na 25.

Bango ambayo ni aina ya bangi inayopatikana katika eneo la Mashariki ya Kati hutumika zaidi lakini hata cocaine,heroine na dawa za kemikali mfano Ecstasy zinatumika kwa wingi kwa mujibu wa utafiti huo.Takriban watoto laki 4 wanatumia dawa za kulevya nchini Misri iliyo mzalishaji,muuzaji na mtumiaji mkubwa wa dawa hizo.

Kulingana na Afisi ya Umoja wa mataifa inayopambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu ,UNODC Misri iko katika njia muhimu ya usafirishaji wa dawa za kulevya kutoka maeneo ya Kusini masharibi mwa Asia na Ulaya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com