CAIRO : Udanganyifu wa kura katika uchaguzi wa bunge | Habari za Ulimwengu | DW | 12.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CAIRO : Udanganyifu wa kura katika uchaguzi wa bunge

Kumekuwepo na madai ya udanganyifu wa kura na vitisho katika uchaguzi wa kwanza wa bunge chini ya katiba mpya nchini Misri.

Imeripotiwa kwamba polisi iliwazuwiya watu kupiga kura katika baadhi ya maeneo ambapo chama cha upinzani cha Muslim Brotherhood kina nguvu kubwa.Wagombea wa chama hicho cha Kiislam katika uchaguzi huo wa baraza la juu la bunge wamelalamika kwamba mashushu wa serikali waliwapiga ndani ya vituo vya kupigia kura na kujaza kura za bandia kwenye visanduku vya kura kabla ya upigaji kura kuanza.

Uchaguzi huo ni kwa ajili ya viti 88 kati ya 176 katika baraza la juu la bunge ambalo lina madaraka makubwa zaidi kwa mujibu wa marekebisho ya katiba yaliodhinishwa hapo mwezi wa Machi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com