Buenos Aires: Bibi Christina Fernandes de Kirchner anatazamiwa kushinda uchaguzi wa urais huko Argentina | Habari za Ulimwengu | DW | 28.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Buenos Aires: Bibi Christina Fernandes de Kirchner anatazamiwa kushinda uchaguzi wa urais huko Argentina

Uchaguzi wa urais umeanza huko Argentina. Mtu anayetazamiwa sana kushinda ni Bibi Christina Fernades de Kirchner, mke wa rais wa sasa, Nestor Kirchner. Uchunguzi wa maoni ya watu unaonesha bibi huyo anaweza kupata wingi unaotakiwa wa kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi. Kuna watetezi 14 wanaowania nafasi hiyo ya juu kabisa katika Argentina. Wapigaji kura pia wanachagua nusu ya wabunge na thuluthi moja ya maseneta. Pia katika mikoa minane kutachaguliwa magavana na mabunge ya mikoa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com