BRUSSELS:Wafanyibiashara wa Ulaya walalamikia mfumko wa bidhaa rahisi kutoka China na Vietnam | Habari za Ulimwengu | DW | 04.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BRUSSELS:Wafanyibiashara wa Ulaya walalamikia mfumko wa bidhaa rahisi kutoka China na Vietnam

Umoja wa Ulaya umekubaliana kutoza ushuru wa ziada viatu vya bei rahisi vinavyoingizwa kutoka China na Vietnam katika mataifa ya Ulaya.

Hatua hii imechukuliwa na Umoja huo ili kuzuia mfumko wa uingizwaji bidhaa za bei rahisi kutoka nchi hizo mbili.

Ushuru huo wa ziada utatozwa katika kipindi cha miaka miwili badala ya miaka mitano kama ilivyotaka tume ya Ulaya.

Nchini Ujerumani kiasi ya asilimia 60 ya viatu vinavyouzwa vinatokea China na Vietnam.Wafanyibiashara nchini humu wanasema uingizwaji wa bidhaa hizo za bei rahisi unaharibu ushindani wa kibiashara.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com