Bonn.Mataifa 80 ya ACP kufaidika na makubaliano ya kibiashara na bara la Ulaya. | Habari za Ulimwengu | DW | 14.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Bonn.Mataifa 80 ya ACP kufaidika na makubaliano ya kibiashara na bara la Ulaya.

Umoja wa Ulaya umesema kuwa unamatumaini ya kukamisha makubaliano mapya ya biashara na kiasi mataifa 80 ya Afrika, Caribbean na Pacific ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Wakati huo unatakuwa muda wa kusamehewa katika makubaliano ya pamoja ya kibiashara na mataifa yanayoendelea na shirika la biashara duniani WTO utakapomalizika .

Kamishna wa masuala ya biashara wa umoja wa Ulaya Peter Mandelson amesema kuwa bila ya kuwa na makubaliano, mataifa ya ACP yanaweza kuwa katika hatari ya kutengwa kutoka katika uchumi wa dunia. Mandelson alikuwa akizungumza katika mkutano wa maendeleo wa umoja wa Ulaya na mawaziri wa biashara wa mataifa ya ACP mjini Bonn, Ujerumani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com