1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Blinken aanza ziara yake China

24 Aprili 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewasili mjini Shanghai, China mapema leo kwa ziara yake ya pili nchini humo katika muda wa chini ya mwaka mmoja. Suala la China kuisadia Urusi litajadiliwa pia

https://p.dw.com/p/4f8CH
Blinken/ China
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewasili leo mjini Shanghai, ChinaPicha: Mark Schiefelbein/AP//Pool AP/dpa/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewasili mjini Shanghai, China mapema leo kwa ziara yake ya pili nchini humo katika muda wa chini ya mwaka mmoja. Mazungumzo magumu yanatarajiwa kufanyika kati ya mataifa hayo yenye uchumi mkubwa zaidi duniani ikiwemo suala la China kuiunga mkono Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine. 

Soma zaidi: Marekani yasema Ukraine itajiunga na NATO

Blinken amewasili mapema leo mjini Shanghai ambapo pamoja na kufanya mazungumzo na viongozi wa China waziri huyo pia atakutana na viongozi wa kibiashara pamoja na vijana katika kile msaidizi wake amekiita kuangazia uhusiano rafiki wa watu wa Marekani na China.

Ziara ya Blinken inalenga kuimarisha mahusiano baina ya mataifa hayo wakati ambapo mvutano kati ya mataifa hayo yenye uchumi mkubwa duniani ukipungua tangu alifanya ziara yake ya mwisho mwezi juni mwaka uliopita.

Ziara ya pili China kwa Blinken

Mwaka uliopita Blinken alikuwa kiongozi wa ngazi ya juu zaidi wa Marekani kuitembelea China katika kipindi cha miaka mitano na baada ya safari yake hiyo marais wa mataifa hayo mawili Xi Jinping wa China na Joe Biden wa Marekani walikutana mwezi Novemba.

Katika mkutano huo wa kilele wa marais hao wawili huko California Xi Jingping alikubali orodha ya matakwa ya Marekani ikiwemo kurejesha mawasiliano ya kijeshi baina ya mataifa hayo na kushirikiana katika masuala ya udhibiti wa dawa za kemikali.

Xi Jingping
Rais wa Chuina Xi JinspingPicha: Kay Nietfeld /AFP

Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa Marekani anayetazama safari ya Blinken amesema kuwa Marekani na China zipo uhusiano mzuri tofauti na kipindi cha mwaka mmoja uliopita ambapo uhusiano baina ya mataifa hayo mawili ulikuwa kwenye hali mbaya ya kihistoria.

Soma zaidi: Blinken atarajiwa kufanya ziara Ufaransa na Ubelgiji kujadili mizozo ya Ukraine na Gaza

Lakini pamoja na kutajwa kuimarika kwa  mahusiano hayo bado utawala wa Biden unasimama kinyume na China baada ya hivi karibuni Marekani kuituhumu China inaisadia Urusi vifaa vya kijeshi na teknolojia katika vyake dhidi ya Ukraine.

Wiki iliyopita, Blinken aliwahimiza viongozi wa Ulaya akiwemo Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz aliyezuru Beijing hivi majuzi, kusimama kidete na kutoiunga mkono China kwa sababu inashirikiana na kuipa nguvu Urusi ya kupambana na Ukraine.

Rais Joe Biden/ Marekani
Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Alex Brandon/AP/dpa/picture alliance

"Ikiwa China inalenga kwa upande mmoja kutaka uhusiano mzuri na Ulaya na nchi nyingine, haiwezi tena kwa upande mwingine ikawa inachochea kile ambacho ni tishio kubwa kwa usalama wa Ulaya tangu kumalizika kwa Vita Baridi.Na sio lazima uyaamini hayo ninaysome lakini ndio niliyoyasikia kwenye mkutano wa G7'' alisema Blinken kwenye mkutano wa mataifa tajiri duniani huko Italia.

Soma zaidi: Blinken awasili Israel katika juhudi za kutatua mzozo wa vita

Wakati Blinken akiwa ziarani nchini China, Marekani kwenyewe leo Rais Joe Biden anatarajiwa kusaini muswada wa program ya TikTok ama iondolewe katika kampuni mama ya China ya ByteDance ama ifungiwe katika soko la Marekani na kwa muda mrefu suala hilo limeongeza mvutano baina ya mataifa hayo.

Mwandishi: Suleman Mwiru
Vyanzo: AFP & Reuters