1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cameron awasili Washington kujadiliana Ukraine, Gaza

Mohammed Khelef
10 Aprili 2024

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uingereza, David Cameron, alitazamiwa kukutana na mwenzake wa Marekani, Antony Blinken, siku ya Jumanne (Aprili 9) wakati wa ziara yake mjini Washington kuzungumzia vita vya Ukraine na Gaza.

https://p.dw.com/p/4eYx0
Baerbock, Blinken na Cameron
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uingereza, David Cameron (kulia), na mwenzake wa Marekani, Antony Blinken (kushoto) wakiwa na mwenzao wa Ujerumani, Annalena Baerbock.Picha: Bruna Prado/AP/picture alliance

Kabla ya mazungumzo yake na Blinken, Cameron angelikutana na rais wa zamani, Donald Trump, kwenye makaazi yake ya Florida, katika kile kilichotajwa kuwa ni "jambo la kawaida" kukutana na mgombea wa upinzani,  kwa mujibu wa msemaji wa ofisi yake.

Soma zaidi: Cameron aelekea Berlin kujadili mizozo ya Ukraine na Gaza

Wiki iliyopita, Cameron alisema angelionana na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani kutokea chama cha Republican, Mike Johnson, na kumshawishi aidhinishe kitita cha dola bilioni 60 cha msaada wa kijeshi kwa Ukraine, ambao umezuiliwa kwa miezi kadhaa sasa na Baraza hilo.