1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken atarajiwa wiki ijayo kufanya ziara barani Ulaya

28 Machi 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anatazamiwa wiki ijayo kufanya ziara barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/4eChY
 Antony Blinken akiwasili  Israel
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alipokuwa akiwali nchini Israel:22.03.2024Picha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller amesema kuwa Blinken ataelekea mjini Paris na kukutana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron  na kujadili kuhusu msaada kwa Ukraine, juhudi za kuzuia kuongezeka kwa mzozo wa Gaza, na masuala mengine muhimu.

Baadaye Aprili mosi hadi tano, Blinken ataelekea mjini Brussels nchini Ubelgiji ili kudhihirisha jukumu la Marekani katika Jumuiya ya Kujihami NATO, kuimarisha ushirikiano na kujadili namna ya kushughulikia changamoto za kimataifa.

Mnamo Aprili 4,   Mawaziri wa mambo ya nje wa NATO  watajumuika katika sherehe za kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ya kujihami ya NATO. Blinken atalitembela pia jiji la Ubelgiji la Leuven, ambapo atahudhuria mkutano wa Baraza la Biashara na Teknolojia la Umoja wa Ulaya na Marekani.