Bernard Kouchner aalikwa na Hamas Ukanda wa Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 24.05.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Bernard Kouchner aalikwa na Hamas Ukanda wa Gaza

-

Serikali ya chama cha Hamas inayotawala ukanda wa Gaza imemualika waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Bernard Kouchner kutembelea eneo hilo ajionee madhila wanayoyapata wapalestina wanaoishi Gaza.Msemaji wa Hamas amefahamisha kwamba wamemualika waziri Kouchner kutokana na msimamo wa Ufaransa wa kimaadili ambao umeonekana kupitia matamshi ya waziri huyo.Kouchner ambaye amekuwa akifanya ziara Israel na Ukingo wa Magharibi tangu jumanne amekosoa hatua ya Israel ya kujenga makaazi zaidi ya walowezi wa kiyahudi katika eneo la ukingo wa magharibi na pia vizuizi vya barabarani vilivyowekwa na nchi hiyo kuwanyima uhuru wa kutembea wapalestina.Awali mwanadiplomasia huyo wa Ufaransa alithibitisha ripoti kwamba afisa mmoja mstaafu wa Ufaransa amekuwa akiwasiliana na kundi la Hamas licha ya Marekani na Umoja wa Ulaya kulisusia kundi hilo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com