1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Juhudi za kuishawishi Iran zitaendelea

6 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuX

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank- Walter Steimier amesema kuwa mazungumzo baina yake na mpatanishi mkuu wa maswala ya nyuklia wa Iran Ali Larijani hayakuzaa matunda kuhusiana na mpango wa nyuklia wa Iran.

Steinmier hata hivyo amesema juhudi za kuishawishi Tehran kuachana na mpango wake wa kurutubisha madini ya Uranium zitaendelea.

Baraza la usalama la umoja wa matiafa limetishia kuiwekea vikwazo zaidi Iran iwapo itaendelea na mpango wake wa kinyuklia.