BERLIN:Bundestag lajadili juu ya kuongeza muda wa vikosi Afghanstan | Habari za Ulimwengu | DW | 01.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN:Bundestag lajadili juu ya kuongeza muda wa vikosi Afghanstan

Bunge nchini Ujerumani Bundestag linajadili juu ya kuongeza muda wa kubakia kikosi cha Ujerumani huko Afghanstan pamoja na kutuma ndege za kivita.

Wizara ya ulinzi imesema jeshi la Ujerumani halitahusika moja kwa moja kwenye mapambano lakini viongozi wa upinzani wanapinga suala hilo.

Bunge linatarajiwa kufikia uamuzi juu ya iwapo watatuma ndege hizo katika wiki zijazo.Mswaada huo hata hivyo unatarajiwa kupita kwani serikali ya mseto ina idadi kubwa ya viti bungeni.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com