BERLIN : Wapelelezi wa Uingereza kuchunguza Hamburg | Habari za Ulimwengu | DW | 11.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Wapelelezi wa Uingereza kuchunguza Hamburg

Mpelelezi kutoka shirika la upelelezi la Uingereza la Scotland Yard anatazamiwa kuungana na maafisa polisi wa Ujerumani wanaochunguza kuwepo kwa uwezekano wa uhusiano kati ya mji wa Hamburg nchini Ujerumani na kuuwawa kwa sumu kwa mpelelezi wa zamani wa Urusi Alexander Litvinenko.

Polisi ya Ujerumani imegunduwa ishara za sumu ya miale ya nuklea ya plutonium 210 kwenye nyumba na kwenye gari lililotumiwa na mfanya biashara wa Urusi Dimitry Kovtun mjini Hamburg.Kovtun ni mmojawapo ya Warusi wawili waliokutana na Litvinenko kwenye hoteli moja huko London hapo Novemba Mosi siku ambayo aliiguwa.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ameitaka serikali ya Urusi kufanya kile iwezalo kusaidia kutowa ushirikiano wao juu ya suala hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com