BERLIN: Wajerumani washerehekea siku kuu ya muungano wa taifa | Habari za Ulimwengu | DW | 03.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Wajerumani washerehekea siku kuu ya muungano wa taifa

Ujerumani imesherehekea leo siku kuu ya muungano wa taifa ambapo sasa ni mwaka wa 16 tokea iliokuwa sehemu ya kikoministi Ujerumani ya mashariki kujiunga na sehemu ya magharibi na kuwa taifa mmoja.

Ma mia kwa maelfu ya watu wamekusanyika katika mji wa Kiel kaskazini mwa Ujerumani, wakihudhuria pia rais Horst Köhler na Kansela Angela Merkel.

Kansela Merkel amesema kuwa siku ya leo ni siku maalum:

´´Kwa mtu kama mimi, mwanamke kutoka Ujerumani ya mashariki kuweza kuwa Kansela wa Ujerumani katika Ujerumani iliyoungana, kwangu mimi baada ya miezi 10 madarakani, sasa ni jambo la kawaida. Lakini katika siku kama hii ya leo ni kitu kisichokuwa cha kawaida. Kitu hicho kinaonyesha Ujerumani ya leo´´.

Wakati ukisherehekewa muungano wa taifa, waziri wa maendeleo kwa ajili ya eneo la mashariki mwa Ujerumani, amesema kwamba ingawaje kuna maendeleo fulani yameshafikiwa, hata hivyo eneo la mashariki litahitaji misaada ya kifedha kutoka eneo la magharibi kwa muda wa miaka kati ya 15 na 20 ijayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com