1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Rais Köhler aanza ziara yake kaskazini mwa Afrika

11 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBK1

Rais wa Ujerumani Hosrt Köhler anaanza ziara yake katika nchi za Afrika Kaskazini hii leo. Kiongozi huyo anaandamana na waziri wa misaada ya maendeleo wa Ujerumani, Heidermarie Wieczoreck-Zeul.

Kituo cha kwanza cha ziara hiyo ni nchini Algeria ambako viongozi hao watahudhuria mkutano wa kundi la nchi nane kuhusu ushirikiano na bara la Afrika.

Wakati wa ziara yao ya wiki nzima, rais Horst Köhler na waziri Heidermarie Wieczoereck-Zeul wataitembelea Mauritania na Malta.