BERLIN: Peres aisifu Ujerumani kwa kutuma wanamaji kulinda pwani ya Lebanon | Habari za Ulimwengu | DW | 05.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Peres aisifu Ujerumani kwa kutuma wanamaji kulinda pwani ya Lebanon

Makamu waziri mkuu wa Israel, Shimon Peres, ameisifu Ujerumani kwa kutuma meli za jeshi la wanamaji kulinda usalama katika pwani ya Lebanon.

Akizungumza wakati wa ziara yake rasmi mjini Berlin, Perez aliwaambia waandishi habari kuwepo kwa wanamaji wa Ujerumani katika pwani ya Lebanon kutasaidia kupunguza idadi ya silaha zinapolekewa wanamgambo wa Hezbollah.

Wakati huo huo, meli nane za kwanza za Ujerumani zikiwa na wanajeshi takriban 1,000 zilitia nanga katika bandari ya Cyprus hapo jana. Ukaguzi wa awali katika pwani ya Lebanon umepangwa kuanza hii leo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com