Berlin. Mwanaanga wa Ujerumani arejea duniani. | Habari za Ulimwengu | DW | 24.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Berlin. Mwanaanga wa Ujerumani arejea duniani.

Rais wa Ujerumani Horst Koehler amempongeza rasmi mwanaanga wa Ujerumani Thomas Reiter baada ya kurejea duniani kufuatia kuishi kwa muda mrefu katika kituo cha kimataifa cha anga ISS.

Reiter aliwasili usiku wa Ijumaa katika eneo la Cape canaveral, Florida, katika chombo cha anga cha Marekani Discovery baada ya kukaa kwa muda wa siku 172 katika kituo hicho cha anga cha kimataifa katika ujumbe wa shirika la anga la Ulaya ESA. Wakati akiwa katika kituo hicho, Reiter alifanya utafiti mara 33 kwa niaba ya shirika la anga la Ulaya na kutembea angani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com