BERLIN ; Mhandisi wa Kijerumani aachiliwa Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 10.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN ; Mhandisi wa Kijerumani aachiliwa Afghanistan

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir ameelezea kufarajika kwake baada ya mhandisi wa Kijerumani na wananchi wanne waliokuwa wakiandamana naye kuachiliwa huru baada ya kutekwa nyara nchini Afghanistan tokea mwezi wa Julai.

Gavana wa wilaya katika mji wa Ghazni Mohammed Naeem amesema watu hao watano walibadishwa na wafungwa watano wa Taliban.Katika taarifa fupi Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 62 Rudolf Blechshmidt amesema yuko katika afya njema lakini amechoka.Mhandisi huyo anatazamiwa kupelekwa kwenye ubalozi wa Ujerumani mjini Kabul.

Blechschmidt na Mjerumani mwenzake Rüdiger Dietdrich walitekwa nyara hapo Julai 18 katika jimbo la Wardak.

Waasi wa Taliban walimuuwa kwa kumpiga risasi Diedrich baada ya kuuguwa wakati akiwa kizuizini.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com