BERLIN : Mgomo wa waongoza safari za ndege haupo kwa sasa | Habari za Ulimwengu | DW | 06.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Mgomo wa waongoza safari za ndege haupo kwa sasa

Tishio la mgomo wa wafanyakazi wa mnara wa kuongoza safari za ndege katika viwanja vya ndege nchini Ujerumani linaonekana kwa hivi sasa limeepukwa.

Uongozi na Umoja wa vyama vya wafanyakazi ambao unawakilisha wafanyakazi hao wa kuongoza safari za ndege wameonyesha ishara ya kuwa tayari kuingia kwenye suluhisho katika juhudi za kuutatuwa mzozo huo.

Mapema umoja wa vyama vya wafanyakazi ulikataa pendekezo la uongozi la kupandisha mishahara kwa asilimia 3 badala ya asilimia 4 inayodaiwa na wafanyakazi.

Chini ya mchakato wa usuluhishi hakutakuwepo na wito wa kugoma kwa takriban siku 14.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com