BERLIN : Mgomo wa reli wanukia | Habari za Ulimwengu | DW | 01.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Mgomo wa reli wanukia

Kuna uwezekano wa kutibuliwa kwa shughuli za usafiri wa reli nchini Ujerumani wakati vyama viwili vya wafanyakazi vyenye kuwawakilisha wafanyakazi wa reli vikitafakari kufanya migomo ya tahadhari.

Shirika kuu la reli nchini la Deutsche Bahn limekataa madai ya vyama vya wafanyakazi kupandisha mishahara ya wafanyakazi 134,000 kwa asilimia saba.Badala yake imekubali kupandisha mishahara hiyo kwa asilimia mbili.

Madereva wa treni pia wametishia kugoma.Chama cha wafanyakazi cha GDL kinadai ongezeko la mishahara la hadi asilimia 31 na kwamba uongozi umekuwa na makubaliano tafauti ya malipo hayo ya mishahara kwa ajili ya madereva.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com