BERLIN : Mfuko wa fidia ya watumwa wa kazi wapongezwa | Habari za Ulimwengu | DW | 13.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN : Mfuko wa fidia ya watumwa wa kazi wapongezwa

Viongozi wa Ujerumani wamefanya kumbukumbu ya kumalizika kwa kazi ya mfuko ulioanzishwa kuwafidia watumwa wa kazi katika enzi ya Manazi nchini Ujerumani.

Mfuko huo ulianzishwa miaka saba iliopita.Fedha za mfuko huo zilitoka katika serikali na makampuni kama vile Volkswagen Daimler Chrysler,Bayer na Deutsche Bank ambayo yote yalikuwa yamewaajiri watumwa na kutumikisha watu kwa nguvu.Kampuni zilizotowa michango yao kwenye mfuko huo zilipewa kinga dhidi ya madai ya kisheria kuhusiana na suala hilo.

Kansela Angela Merkel na Rais Horst Köhler wa Ujerumani waliongoza kumbukumbu hiyo mjini Berlin na kusifu kazi ya mfuko huo kwa kusema kwamba ulipaji wake fidia wa kiishara ulikuwa ni wajibu wa kimaadili wa Ujerumani.

Watumwa wa kazi wanaokadiriwa kufikia milioni 10 walilazimishwa kufanya kazi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Wahanga wasiozidi milioni mbili wamenufaika na mpango huo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com