BERLIN: Madereva wa treni watishia kugoma kazi tena | Habari za Ulimwengu | DW | 13.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BERLIN: Madereva wa treni watishia kugoma kazi tena

Madereva wa treni nchini Ujerumani huenda wakagoma kazi tena siku ya Jumatano,ikiwa shirika la reli la Ujerumani-Deutsche Bahn-hii leo halitotoa pendekezo bora la nyongeza ya mshahara. Kwa mara ya kwanza,Kansela Angela Merkel ameingilia kati mgogoro huo na amezihimiza pande zote mbili kujadiliana upya.Akawaonya kuwa migomo zaidi huenda ikaathiri uchumi wa nchi vibaya sana.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com