1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Madereva wa treni kugoma.

2 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBL1

Chama cha madereva wa treni nchini Ujerumani kimewataka wanachama wake kufanya mgomo kuanzia siku ya Ijumaa. Wito huo unakuja baada ya kushindwa kwa mazungumzo ya ongezeko la mshahara na kampuni inayomilikiwa na taifa ya Deutsche Bahn.

Chama cha madereva wa treni kilikuwa kinadai ongezeko la asilimia 30 mbali na ongezeko la asilimia 4.5 lililokubaliwa na vyama viwili vingine ambavyo vinawakilisha idadi kubwa ya madereva wa shirika hilo la Deutsche Bahn. Licha ya uwezekano wa mgomo huo , zaidi ya nusu ya treni za Ujerumani zinatarajiwa kusafiri. Gazeti la Bild am Sonntag limeripoti siku ya Jumapili kuwa Deutsche Bahn linapanga kuomba madereva wa treni kutoka Austria na Uswisi ili kuzuwia athari za mgomo huo.