BEIRUT: Wanamaji wa Ujerumani watakamilisha ujumbe wao | Habari za Ulimwengu | DW | 29.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIRUT: Wanamaji wa Ujerumani watakamilisha ujumbe wao

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung,amesema vikosi vya wanamaji wa Kijerumani wanaoshiriki katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa kulinda pwani ya Lebanon,watashiriki katika utaratibu huo wa amani katika Mashariki ya Kati mpaka mwisho.Waziri Jung alitamka hayo wakati wa ziara yake katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut. Ujumbe wa hivi sasa wa vikosi vya wanamaji wa Kijerumani nchini Lebanon,unamalizika Septemba mwaka 2008.Kiasi ya wanamaji 750 wa Kijerumani, kama sehemu ya vikosi vya kimataifa,wanapiga doria nje ya pwani ya Lebanon,ili kuzuia usafirishaji haramu wa silaha.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com