BEIRUT: Maandamano makubwa ya kundi la Hezbollah yafanyika | Habari za Ulimwengu | DW | 23.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BEIRUT: Maandamano makubwa ya kundi la Hezbollah yafanyika

Mamia ya Walebanon wanafanya maandamano makubwa katika barabara za mjini Beirut hii leo. waandamanaji wamezifunga barabara kubwa kufuatia mgomo wa siku moja ulioitishwa na kundi la upinzani la wanamgambo wa Hezbollah.

Kundi hilo linaloungwa mkono na Syria limeitisha mgomo huo makusudi kuendeleza mgomo wake baridi nje ya ofisi za serikali katika juhudi za kuipindua serikali na kuishinikiza serikali ya waziri mkuu Fouad Siniora ijiuzulu.

Migomo baridi iliyopangwa na kundi la Hezbollah tangu Disemba mosi mwaka jana, imeshindwa kuiondoa madarakani serikali. Waziri mkuu Fouad Siniora amewataka Walebanon waupuuze mgomo huo wa leo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com