BAGHDAD:Kinara wa mashambulizi ya kuvizia Iraq auawa | Habari za Ulimwengu | DW | 22.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Kinara wa mashambulizi ya kuvizia Iraq auawa

Majeshi ya Marekani huko Iraq yamesema kuwa yamefanikiwa kumuua mtu ambaye anaaminika kuwa ni mpangaji wa mashambulizi ya kuvizia ya hivi karibuni ambapo yamepelekea wanajeshi watano wa Marekani kuawa.

Azhar al Dulaimi aliuawa hapo siku ya Ijumaa katika mapigano wakati majeshi ya Marekani yalipokuwa yakijaribu kumkamata, huko Kaskazini mwa Baghdad

Msemaji wa Jeshi la Marekani Meja Jenerali William Caldwell amesema kuwa Dulaimi anaaminika kuwa kiongozi wa mashambulizi ya kambi ya majeshi hayo huko Karbala ambapo askari mmoja aliuawa na wengine wanne walitekwa kabla ya kuuawa baadaye.

Majeshi ya Marekani yamekuwa yakimsaka Dulaimi toka shambulizi hilo la January lililopangwa kitaalam, wakati watu waliyokuwa wakizungumza kiingereza na wakiwa na silaha na sare za jeshi la Marekani walipoivamia kambi hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com