BAGHDAD : Rais wa Iraq aisakama ripoti ya Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 10.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD : Rais wa Iraq aisakama ripoti ya Marekani

Rais Jalal Talabani wa Iraq ameshutumu vikali matokeo ya utafiti wa jopo la vigogo waandamizi wa Marekani lenye kupendekeza mabadiliko ya msingi kwa sera ya Marekani kwa Iraq.

Talabani amewaambia waandishi wa habari kwamba repoti hiyo sio ya haki na itadhoofisha haki ya Iraq kujiamulia mambo yake yenyewe.Amesema repoti hiyo inaonekana kama vile imeandikwa kwa taifa changa koloni dogo kwa kuwekewa masharti na kupuuza ukweli kwamba nchi hiyo ni huru.

Kwa ujumla Rais huyo ameikataa repoti hiyo kwa kuwa sio tu ya haki bali vifungu vyake pia vinahatarisha uhuru wa kujiamulia mambo yake Iraq pamoja na katiba yake.

Mapendekezo ya repoti hiyi ni pamoja na kufungamanisha msaada wa mataifa ya magahribi na jinsi ya serikali ya nchi hiyo inavyopiga hatua katika suala la usalama na kuwahusisha wanachama wa chama cha Baath cha Rais wa zamani wa nchi hiyo Saddam Hussein katika mchakato wa usuluhishi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com