BAGHDAD: Mashambulio ya Marekani yamelenga vituo vya waasi | Habari za Ulimwengu | DW | 04.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Mashambulio ya Marekani yamelenga vituo vya waasi

Wanajeshi wa Kimarekani nchini Irak wamesema mashambulio ya angani yaliofanywa ndani na ukingoni mwa mji mkuu Baghdad yamewaua wanamgambo wa ngazi ya juu walioshukiwa kuzilenga helikopta za Marekani.Vile vile,idadi fulani ya wafuasi wa mtandao wa Al Qaeda waliyohusika na mashambulio ya kuripua mabomu ya gari waliuawa katika operesheni hiyo.Wakati huo huo si chini ya watu 12 wameuawa na zaidi ya 20 wamejeruhiwa katika shambulio la kujitolea muhanga,lililofanywa karibu na mji wa Ramadi,magharibi mwa nchi.Kwa mujibu wa polisi,shambulio hilo lilifanywa siku ya Jumamosi kwenye kituo cha ukaguzi,nje ya mji. Vile vile katika mji wa Yusufiya,familia ya watu 6 wa madhehbu ya Kisunni waliuawa na waasi.Wakati huo huo bomu lililotegwa kando ya barabara,limeua wanajeshi 3 wa Kimarekani katikati ya Baghdad.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com