1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Marekani na Iran zaijadili Iraq.

29 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBx6

Marekani na Iran zimekuwa na majadiliano ya ngazi ya juu kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 27.

Majadiliano hayo katika ngazi ya mabalozi mjini Baghdad yalilenga katika hali ya ghasia nchini Iraq.

Balozi wa Marekani Ryan Crocker ameyaeleza mazungumzo hayo ya saa nne na mwenzake wa Iran Hassan Kazemi kuwa ya manufaa.

Crocker amerudia madai ya Marekani kuwa Iran inasaidia wapiganaji nchini Iraq.

Mwenzake wa Iran , hata hivyo , amelishutumu jeshi la Marekani kwa kutofanya vya kutosha kulipa jeshi la Iraq silaha za kutosha na kusema kuwa jamhuri ya hiyo ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuingilia kati na kulipatia jeshi la nchi hiyo silaha.

Mazungumzo ya jana yaligubikwa hata hivyo na ghasia zaidi. Lori moja lililokuwa na milipuko lililipuka karibu na msikiti mkuu wa Wasunni mjini Baghdad, na kuuwa watu wapatao 24 na kuwajeruhi wengine 70.