BAGHDAD: Irak na Syria zakubaliana kurejesha uhusiano wa kidiplomasia | Habari za Ulimwengu | DW | 22.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Irak na Syria zakubaliana kurejesha uhusiano wa kidiplomasia

Irak na Syria zimekubaliana kurejesha uhusiano wa kidiplomasia ambao ulikatika miaka 25 iliopita. Waziri wa mambo ya kigeni wa Irak, Hoshyar Zebari, ametoa taarifa hiyo wakati yeye pamoja na mwenzake wa Syria Walid Muallem, wakiuhotubia mkutano na waandishi wa habari. Waziri wa mambo ya kigeni wa Syria yuko ziarani mjini Baghdad. Wanadiplomasia hao wawili wamesema wamekubaliana pia kushirikiana kuhusu maswala ya kiusalama.

Uhusiano kati ya Irak na Syria ulivunjika mwaka 1982 wakati wa utawala wa rais Saddam Hussein.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan, amesema hiyo ni hatua ambayo inaweza kusaidia kuleta amani katika eneo zima. Wakati hayo yakiarifiwa, rais wa Irak, Jalal Talabani, anatarajiwa kufanya ziara mjini Teheran nchini Iran mwishoni mwa wiki hii kwa mazungumzo na rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad. Iliarifiwa pia kuwa rais wa Syria, Bashar al- Assad, atashiriki kwenye mazungumzo hayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com