BAGHDAD: Ghasia zaendelea nchini Irak wakati wa ziara ya Rice | Habari za Ulimwengu | DW | 17.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Ghasia zaendelea nchini Irak wakati wa ziara ya Rice

Waziri wa masuala ya nje wa Marekani,Condoleezza Rice amefanya ziara ya ghafula mjini Baghdad.Ziara hiyo imefanywa wakati ghasia mpya zikizuka katika mji wa kaskazini wa Kirkuk.Katika machafuko hayo,miripuko miwili ya gari iliua si chini ya watu 8 na wengine dazeni kadhaa walijeruhiwa.Ndege ya waziri Rice ilipaswa kuzunguka angani mjini Baghdad kwa nusu saa,kabla ya kuweza kutua kwa sababu ya harakati za kijeshi zizlizokuwa zikiendelea katika mji huo mkuu wa Irak.Baadae Rice alaisema vikosi vya Marekani na vya Irak katika operesheni mpya dhidi ya wanamgambo mjini Baghdad,vimefanikiwa kupata maendeleo kadhaa.Kabla ya kukutana na waziri mkuu wa Irak Nouri al-Maliki,Bibi Rice alionana na wanajeshi na maafisa wa Kimarekani.Rice leo anaelekea Israel ambako atakuwa na mkutano wa kilele pamoja na Waziri mkuu wa Israel,Ehud Olmert na Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas mjini Jerusalem.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com