ASTANA: Vyama vya upinzani vyapinga matokeo ya uchaguzi
19 Agosti 2007Matangazo
Chama cha Rais Nursultan Nazarbayev wa Kazakhstan,kimejinyakulia ushindi mkubwa katika uchaguzi wa bunge uliofanywa siku ya Jumamosi.Kwa mujibu wa matoeko ya mwanzo,chama cha rais cha Nur Otan,kimejinyakulia asilimia 88 ya kura zilizopigwa na hivyo kitakuwa chama pekee katika bunge jipya.
Vyama vyote vingine vimeshindwa kuvuka kiwango cha asilimia 7 kinachohitajiwa ili kuweza kuingia bungeni.Vyama vya upinzani vimekataa kutambua matokeo hayo na vinasema,hesabu hizo zimefanyiwa udanganyifu.