1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Asmara. Eritrea yakanusha kuhusika na utekaji nyara raia wa Uingereza.

5 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCME

Eritrea imekanusha kuhusika katika tukio la kukamatwa kwa kundi la raia wa Uingereza katika eneo la kaskazini mashariki ya Ethiopia. Msemaji wa serikali ya Eritrea amesema kuwa shutuma hizo hazina msingi wowote.

Raia hao watano wa Uingereza , ikiwa ni pamoja na mfanyakazi wa ubalozi , na raia 13 wa Ethiopia waliokuwa waongozaji wa kundi hilo wamepotea siku nne zilizopita katika jimbo la Afar.

Imeripotiwa kuwa watano kati ya Waethiopia 13 wamepatikana na majeshi ya usalama karibu na mpaka wa nchi hiyo na Eritrea. Maafisa wa wizara ya mambo ya kigeni wa Uingereza wamewasili katika mji mkuu wa Ethiopia , Addis Ababa, wakati kundi la wanajeshi maalum wa Uingereza linasemekana linajitayarisha.