ANKARA : Waturuki wapiga kura katika uchaguzi wa bunge | Habari za Ulimwengu | DW | 22.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ANKARA : Waturuki wapiga kura katika uchaguzi wa bunge

Waturuki leo wanapiga kura katika uchaguzi wa bunge unaowapambanisha chama tawala cha AK chenye mizizi ya siasa kali za Kiislam dhidi ya wale wenye misimamo ya utaifa ambapo vinatafuatiana sana juu ya mustakbali wa kufuata nchi hiyo.

Uchunguzi wa maoni unaonyesha kwamba Chama cha AK cha Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan kinaweza kuendelea kutawala peke yake miaka mengine mitano lakini suala la wingi wao wa viti bungeni litakuwa muhimu.Waturuki wengi wanahofu kuzuka tena kwa mzozo kati ya chama AK cha Erdogan na jeshi la Uturuki lisilokuwa na mafungamano ya kidini iwapo chama hicho kitajaribu tena kumuweka waziri wa mambo ya nje Abdullah Gul katika wadhifa wa Urais.

Mbali na chama kikuu cha upinzani cha Rebulican ya Wananchi na kile cha sera kali za mrengo wa kulia cha MHP wagombea kadhaa wa kujitegemea wanaotetea Wakurdi pia wanashiriki uchaguzi huu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com