Afrika Kusini yaadhimisha miaka 20 tangu Nelson Mandela aachiwe huru | Matukio ya Kisiasa | DW | 11.02.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Afrika Kusini yaadhimisha miaka 20 tangu Nelson Mandela aachiwe huru

Hii leo inaadhimishwa miaka 20 tangu rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, mzee Nelson Mandela, aachiwe huru kutoka jela ya kisiwa cha Robin ambako alizuiliwa kwa miaka 27.

Nelson Mandela na mke wake Winnie baada ya kuachiwa huru hapo Februari,1990.

Nelson Mandela na mke wake Winnie baada ya kuachiwa huru hapo Februari,1990.

Kuachiwa kwake ndio uliokuwa ufunguo wa utawala wa walio wengi nchini humo.

Ili kupata picha halisi ilivyo Afrika Kusini leo, Josephat Charo amezungumza na Bwana Isaac Khomu, mwandishi wa habari na mchambuzi wa maswala ya kisiasa nchini humo na kwanza alikuwa na haya ya kusema.

Mtayarishaji: Josephat Charo

Mhariri: Mohammed Abdulrahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com