1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Nelson Mandela

Nelson Mandela alikuwa mwanamapinduzi wa Afrika Kusini aliepambana dhidi ya ubaguzi wa rangi na utengano “Apartheid”, mwanasiasa na mhisani aliehudumu katika nafasi ya rais kuwanzia 1994 hadi 1999.

Alikuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini. Alihudumu pia kama rais wa chama tawala cha Afrika National Congress kuanzia 1991 – 1997. Serikali yake ilijikita zaidi katika kuvunja mfumo wa ubaguzi wa rangi uliyoitawala Afrika Kusini kwa miongo, na aliongoza juhudi za maridhiano kati ya jamii za Waafrika Kusini weusi na watawala wao wa zamani weupe. Mandela alizaliwa Julai 18, 1918 na alifariki dunia Desemba 5, 2013 akiwa na umri wa miaka 95.

Onesha makala zaidi