1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afisa wa zamani katika jeshi la Rwanda ahukumiwa miaka 20 jela

5 Julai 2007

Mahakama ya Ubelgiji imepitisha hukumu hiyo dhidi ya Meja Bernard Ntuyahaga aliyekutwa na hatia ya kuua wanajeshi 10 wa kulinda amani wa Ubelgiji

https://p.dw.com/p/CB32

Mahakama ya Ubelgiji imemhukumu kifungo cha miaka 20 jela aliyekuwa afisa wa jeshi la Rwanda Meja Bernard Ntuyahaga baada ya kumkuta na hatia ya kuhusika na mauaji ya wanajeshi 10 wa Ubelgiji wa kulinda amani katika kipindi cha mwanzo cha mauaji ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Hata hivyo mahakama haikumkuta na hatia ya kuhusika na mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Rwanda wakati huo bibi Agathe Uwilingiyimana.

Bwana Bernard anaweza kukata rufaa kupinga hukumu hiyo