ABUJA: Mtoto wa miaka mitatu atekwa nyara | Habari za Ulimwengu | DW | 05.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABUJA: Mtoto wa miaka mitatu atekwa nyara

Binti ya mtalaamu mmoja raia wa Uingereza ametekwa nyara leo hii na watu wasiojulikana katika jimbo la Niger Delta nchini Nigeria.

Mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitatu alikuwa akipelekwa shule wakati alipofikwa na mkasa huo wa kunyakuliwa kutoka ndani ya gari.

Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imesema kwamba inachunguza tukio hilo lakini haikutoa maelezo zaidi.

Rais mpya wa Nigeria Umaru Yar’Adua ametoa mwito wa kudumishwa utulivu katika jimbo hilo la Delta.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com