AACHEN : Solana atunukiwa tuzo ya Ujerumani | Habari za Ulimwengu | DW | 17.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

AACHEN : Solana atunukiwa tuzo ya Ujerumani

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Havier Solana ametunukiwa Tuzo ya Charlemagne mojawapo ya tuzo zenye hadhi kubwa za Ujerumani

Nishani hiyo inatambuwa kazi ya Solana katika kushajiisha amani na umoja wa Ulaya.Solana alikabidhiwa tuzo hiyo katika hafla iliofanyika katika mji wa Aachen ulioko kwenye mpaka kati ya Ujerumani,Uholanzi na Ubelgiji.

Tuzo ya Chalmagne ilianzishwa mwaka 1949 kwa kutowa heshima kwa huduma za kutumikia watu na kuleta umoja barani Ulaya.Tuzo hiyo imepewa jina la mfalme wa karne ya nane Charlemagne ambaye alitawala himaya karibu ya eneo zima la ulaya magharibi.

Washindi waliopita wa tuzo hiyo ni pamoja na Wiston Churchil aliekuwa waziri mkuu wa Uingereza,rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton na Papa John Paul wa Pili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com