Ziara ya kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni barani Afrika | Matukio ya Kisiasa | DW | 16.03.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Ziara ya kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni barani Afrika

Papa Benedikt wa 16 aanza ziara ya siku sita kwa kuitembelea Kamerun

KIongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni

KIongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni


Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni, Benedikt wa 16, anaanza hii leo ziara yake ya kwanza barani Afrika tangu alipokabidhiwa wadhifa huo. Na hata kama atazitembelea Angola na Kameroun tuu, Wakristo katika bara zima la Afrika wanamshangiria.


Kameroun inajikuta katika hali ya tahadhari. Katika mji mkuu, Yaounde, vikosi vya usalama vimeanza kubomowa vibanda vya maduka vilivyojengwa bila ya ruhusa.Wafanyabiashara kadhaa wamepoteza walixchokua nacho.Lakini hayo hayamshughulishi mtu yeyote.Hadi leo mchana mji wa Yaounde unabidi uwe safi.Huko ndiko Papa atakakotuwa.Baada ya miaka minne madarakani, kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni, Benedikt wa 16, anaanza hii leo ziara yake ya kwanza barani Afrika. Kila mkamerun mmoja kati ya wanne ni mkatoliki na furaha ni kubwa kupita kiasi miongoni mwa wafuasi wake. Kardinal Francis Arinze wa kutoka nchi jirani ya Nigeria anaelezea kupitia Radio Vatikan, kituo rasmi cha matangazo cha Papa mjini Roma, jinsi waatu wanavyofurahikia ziara ya Papa Benedikt wa 16.


""Wanajua kwamba baba yao yuko mjini Roma, lakini atakapokanyaga ardhi ya Afrika atakua karibu nao zaidi.Watakutana nae,watamuona na watamsikia.Na yeye pia atakutana nao,ataonana nao na kuwasikiliza pia.Na hilo ndio muhimu."


Zaidi ya hayo ziara ya Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni ni ziara ya kuwatanabahisha watu kwasababu Afrika linaangaliwa kama bara ambako kanisa lina nafasi ya kukua. Idadi ya waumini inaaongezeka tangu miaka kadhaa iliyopita. Mnamo mwaka 2007 idadi hiyo iliongezeka kwa asili mia 3. Kulinganisha na mabara mengine, hiyo ni idadi kubwa kabisa ya waumini. Hadhi ya kanisa katoliki nayo pia ni kubwa. Kwa miaka kadhaa sasa kanisa limekua likichangia katika sekta ya maendeleo.


Shule, hospitali, vituo vya kuwatunza wasiojiweza na hasa katika maeneo ya mashambani ni sekta ambazo kanisa limekua likizisaidia serikali nyingi za Afrika. Hata hivyo, makanisa huru yamekua yakiongezeka tangu miaka ya 80. Makanisa hayo yanaangaliwa kama kishindo kwa wakatoliki. Makanisa mengi kama hayo yanachipuka kutokana na msaada ya fedha wa kutoka Marekani.


Askofu Stephen Hippler wa Capetown nchini Afrika kusini anasema amekua akiangalia kwa jicho la hofu jinsi makanisa hayo yanayogharimiwa kutoka Marekani yanavyoenea barani Afrika. Anakosoa "ahadi za uwongo zinazotolewa pamoja na kuwahadaa watu kila watakapochanga pesa nyingi ndipo watakapozidi kutajirika."


Katika ziara yake hii nchini Angola na Kameroun, kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Benedikt wa 16 hatazamiwi kuzungumzia kinaga ubaga kuhusu HIV na Ukimwi.Knyume lakini na mtangulizi wake JOhannes Paulo wa Pili,Papa benedikt wa 16 sio tuu ataopngoza misa kubwa hadharani,bali pia anatazamiwa kuitembelea paraosi moja ndogo.Ziara ya Papa Benedikt wa 16 itadumu siku sita barani Afrika.


Mwandishi: Kriech/Hamidou (ZR)

Mhariri: Miraji Othman
 • Tarehe 16.03.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HDeK
 • Tarehe 16.03.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HDeK
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com