1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WIESBADEN:Viongozi wa Ujerumani na urusi wakamilisha mazungumzo yao

15 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7FZ

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais Vladimir Puttin wa Urusi wamekamilish mazungumzo yao mjini Wiesbaden magharibi mwa Ujerumani.

Viongozi hao wamejadili masuala ya uhusiano kati ya nchi zao katika sekta za uchumi, biashara, sayansi na teknolojia.

Akizungumzia juu ya ushirikiano huo rais Puttin amesema katika historia, Urusi na Ujerumani hazijawahi kukaribiana kama ilivyo hivi sasa.

Mawaziri 12 wa Urusi wameshiriki na wenzao wa Ujerumani kwenye mazungumzo ya mjini Wiesbaden.

Wakati huo huo rais Vladimir Puttin amethibitisha kuwa atafanya ziara nchini Iran licha ya habari za hapo awali juu ya njama za kutaka kumwuua.