Waziri wa ushirikiano wa maendeleo bibi Heidemarie Wieczorek-Zeul atembelea Afrika | Matukio ya Kisiasa | DW | 04.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Waziri wa ushirikiano wa maendeleo bibi Heidemarie Wieczorek-Zeul atembelea Afrika

Waziri wa ushirikiano wa maendeleo bibi Heidemarie Wieczorek-Zeul wa Ujerumani leo anatarajiwa kuwasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kuanza ziara barani Afrika ambapo pia itaitembelea Ethiopia.

Heidemarie Wieczorek- Zeul

Heidemarie Wieczorek- Zeul

Kituo cha kwanza cha ziara ya waziri huyo ni Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo nchi ambayo hivi karibuni ilifanya uchaguzi baada ya miaka mingi ya vita na vurumai.

Bibi Heidemarie Wieczorek atazingatia suala la ujenzi mpya wa nchi hiyo katika mazungumzo yake na viongozi wa JKK.

Amesema atajadiliana na wenyeji wake jinsi juhudi za ujenzi mpya zinavyosonga mbele katika medani ya siasa vilevile. Pia ataangalia jinsi Ujerumani itakavyosaidia katika harakati za kupambana na ukimwi ili kuokoa maisha .

Waziri huyo wa Ujerumani pia amesema kuwa katika mazungumzo yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo atazungumzia juu ya mchango unaoweza kutolewa na nchi yake katika kuweka utaratibu wa kuonesha wazi jinsi raslimali za nchi hiyo zinavyotumika ili kuepusha utajiri huo kutumika na makundi ya waasi kwa ajili ya kununulia silaha.

Waziri wa Ujerumani wa ushirikiano wa maendeleo bibi Heidemarie Wieczorek Zeul pia ataitembelea Ethiopia.

AM.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com